Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichojiri kesi ya vigogo wa NSSF

80224 Pic+nssf

Wed, 16 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya wafanyakazi tisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) nchini Tanzania akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Jamila Vullu umedai upelelezi haujakamilika.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh2 bilioni.

Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai leo Jumanne Oktoba 15, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu, Vick Mwaikambo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa hivyo wanaendelea na upelelezi.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 28, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Vulu wengine ni Mhandishi wa Hundi, Abdulrahaman Njozi, Meneja Uhakiki, Amiri Kapera, Mhasibu Mwandamizi, James Oigo, Mhasibu Mkuu, Hellen Peter, Mhasibu kitengo cha Madeni, Invonne Kimaro, Mhasibu dawati la Uchunguzi, Restiana Lukwaro, Kaimu Rasilimali watu, Tikyeba Alphonce na Mhasibu, Dominic Mbwete.

Inadaiwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 maeneo Dar es Salaam washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani walikula njama na kutakatisha fedha kiasi cha zaidi ya Sh2 bilioni wakiharibu kuonyesha hundi hizo halali zimetolewa na bodi ya wadhamini ya NSSF huku wakijua si kweli.

Pia Soma

Advertisement
Katika shtaka la pili kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 wakiwa Katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa Njozi na Kapera kwa nia ya kufanya udanganyifu walighushi jumla ya hundi 47 za benki ya CRDB ambazo ni akaunti namba 01J1028249500 ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

Shtaka la tatu tarehe hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote wakiwa watumishi wa umma walioajiliwa mliiba jumla ya zaidi ya Sh2 bilioni Mali ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

Simon alidai katika shtaka la nne tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote wakiwa watumishi wa umma waliisababishia hasara NSSF kiasi cha zaidi ya Sh2 bilioni kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Katika staka la tano tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja walijihusisha na miamala haramu ya zaidi ya Sh2 bilioni huku wakifahamu fedha hizo ni mazalio ya kosa tangulizi.

Chanzo: mwananchi.co.tz