Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichojiri kesi ya Wambura wa TFF hiki hapa

61305 Wamburapic

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Upande wa Mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, aliyekuwa  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura, umeieleza Mahakama  unasubiri  taarifa ya maandishi muhimu kutoka kwa mtaalamu wa maandishi.

Wambura anakabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh 100 milioni, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019, iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo, ameieleza Mahakama hiyo, leo Jumanne Juni 4, 2019, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Ndimbo amedai mbele ya Hakimu  Mfawidhi, Kelvin Mhina, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

"Kwa sasa tunasubiri taarifa ya maandishi kutoka kwa mtaalamu wa maandishi ili tuweze kukamilisha upelelezi huu," amedia Maghela.

Ndimbo amedai kutokana na hali hiyo, anaiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Pia Soma

Hakimu Mhina baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, amewataka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo kwa wakati ili hatua nyingine ziweze  kufuata.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 18, 2019 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Kwa mara ya kwanza, Wambura alifikishwa Kisutu, Februari 11, 2019, akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh 100milioni.

Katika mashtaka hayo 17; shtaka moja ni la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo; mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha haramu.

Katika shtaka la kwanza ambalo ni la kughushi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 6, 2004, sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Siku hiyo, Wambura kwa nia ya kutapeli  alitengeneza barua ya  kughushi ambayo haina kumbukumbu namba akionyesha  imeandikwa na E Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa  kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.

Katika shtaka la kutoa na kuwasilisha nyaraka ya uongo, mshtakiwa  alitoa barua iliyokuwa haina kumbukumbu namba  ya Julai 6, 2004, akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na E. Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck System Ltd, akionyesha kuwa anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, kuanzia  shtaka la tatu hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi cha zaidi Sh 95 milioni, kwa njia ya udanganyifu akidai fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbalimbali na riba kutoka kwa kampuni ya Jeck System Ltd huku akijua kuwa siyo kweli.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz