Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichojiri kesi anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma moto hiki hapa

68947 Pic+gavana

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hamisi Saidi (38) ‘Meshack’ ambaye ni mfanyabiashara na Mkazi wa Gezaulole wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuua mke wake Naomi Marijani.

Akisoma hati ya mashitaka leo Jumanne Julai 30, 2019  Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu  Ally Salum amedai mshitakiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la mauaji kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Simon amedai Mei 15, 2019 eneo la Gezaulole wilayani Kigamboni alimuua Naomi Marijani huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Amedai bado wanaendelea na upelelezi  hivyo anaiomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa shauri hilo.

Hakimu Salum  amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hivyo mshtakiwa huruhusiwi kujibu chochote.

Ally ameahirisha shauri hilo hadi Agosti 13, 2019 itakapo tajwa tena.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz