Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana wa miaka 19 mbaroni kwa dawa za kulevya

Ulrich Matei,2 Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia LUSEKELO ELISHA MWAKANGATA mwenye umri wa miaka 19, Mkazi wa Mama John kwa kosa la kupatikana na kete sita sawa na gramu 0.3 za madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni heroin.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 10.02.2022 maeneo ya Mama John, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga jijini Mbeya katika misako inayoendelea maeneo mbalimbali ya Mbeya dhidi ya wahalifu wa matukio mbalimbali.

Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kujihusisha na uuzaji wa dawa hizo za kulevya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live