Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana miaka 19 jela maisha kwa kumbaka mtoto miaka minne

Kijana Miaka 19 Jela Maisha Kwa Kumbaka Mtoto Miaka Minne Kijana miaka 19 jela maisha kwa kumbaka mtoto miaka minne

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha na fidia ya Tsh. milioni 5 Kijana mwenye umri wa miaka 19 Calvin Kahonga baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.

Siku ya tukio Calvin alikwenda nyumba anayoishi Mtoto huyo na kumbaka wakati Mama wa Mtoto alipokwenda kuchota maji na Calvin alipomaliza kufanya tukio hilo alikimbia, Mama wa Mtoto aliporejea aligundua Mtoto wake hayupo sawa ndipo akaenda kutoa taarifa katika ofisi ya Serikali ya Kijiji na taratibu za kumkamata Calvin zikafanyika.

Calvin alipopewa nafasi ya kujitetea Mahakamani hapo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwasababu Mama yake mzazi ni Mlemavu wa mikono na anamtegemea kwa kila kitu lakini Wakili Baton Mayage akaomba Mahakama impe adhabu kali kwakuwa kosa hilo ni la pili na aliwahi kumlawiti Mtoto.

Calvin ambaye ni Mkazi wa Pawag, Isimani Mkoani humo amewahi kuhukumiwa kuchapwa viboko 12 akiwa na umri wa miaka 18 mwaka jana baada ya Mahakama ya Wilaya kumkuta na hatia ya kumlawiti Mtoto wa miaka mitatu.

Kesi hiyo imesimamiwa na Mawakili wa Serikali Ruben Lubango na Baton Mayage na ilikuwa na Mashahidi watatu ambao ni Mtoto, Mama na Daktari ambapo akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mtuhumiwa amekutwa na hatia kutokana ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo hivyo anastahili adhabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live