Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana miaka 19 ashikiliwa kwa utekaji, ubakaji na ulawiti

812d589483a8df32ab50cbef18da99a2 Kijana miaka 19 ashikiliwa kwa utekaji, ubakaji na ulawiti

Sat, 14 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JESHI la polisi Mkoani Mtwara limemkamata Jabiri Bakari kwa kosa la kujihusisha na uhalifu wa utekaji, ubakaji na kulawiti watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 10 katika wilaya ya Mtwara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Mark Njera amewaambia waandishi wa habari leo kuwa mtuhumiwa huyo mwenye miaka 19 alikamatwa August 12,Mwaka huu maeneo ya Mbae Manispaa ya Mtwara kufuatia msako wa jeshi la polisi uliofanywa.

Kamanda Njera amesema kabla ya kukamatwa na jeshi la polisi, mtuhumiwa aliwadanganya watoto wa kike watatu wenye umri wa miaka nane na saba na mwingine mwenye miaka tisa ambao kwa nyakati tofauti aliwaiba sehemu mbalimbali kwa kuwalaghai kwa njia mbalimbali na kufanikiwa kuondoka nao kwenda kwenye maeneo na kuanzisha makazi ya muda akiwa na watoto hao.

Amesema mnamo Juni 25, mwaka huu mtuhumiwa alimlaghai mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba maeneo ya Mbae Mashariki wilaya ya Mtwara mtoto huyo akiwa anacheza na wenzake na baadae kuondoka naye ambapo mtoto huyo alipatikana baada ya siku tano akiwa amefanyiwa vitendo vya ukatili.

Mnamo Julai 8, maeneo ya Mbae, mtuhumiwa huyo alimchukua tena mtoto wa kike mwingine mwenye miaka saba na kutoweka naye na kwenda kusikojulikana. Mtoto huyo alipatikana Julai 24 akiwa amefanyiwa vitendo vya kikatili.

Na mnamo Augus 6,t mtuhumiwa huyo pia alimchukua mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambaye pia alipelekwa kusikojulikana na mtuhumiwa huyohuyo na kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kwa muhjibu wa kamanda Njera, mtoto huyo alipatikana Agosti 7, kufuatia msako wa jeshi hilo.

Kamanda Njera ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mtwara kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto na kutambua watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili kwa watoto na kutoa taarifa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz