Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana jela miaka 20 hujuma miundombinu ya TANESCO

Ce3bfaef81b2250e03a0053412c5181d Kijana jela miaka 20 hujuma miundombinu ya TANESCO

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Tanga imemhukumu Mahamoud Hamis (30) kwenda jela miaka 20 baada ya kumkuta na hatia ya kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Akisoma hukumu jana, Hakimu Husna Majani alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wengine wenye tabia ya kuhujumu miundombinu na kuisababishia serikali na shirika hasara.

Awali mwendesha mashitaka, Joseph Makene alidai Hamis ni miongoni mwa watu waliokamatwa katika operesheni iliyofanywa na Tanesco kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Hujuma hizo za miundombinu ya shirika zilisababisha ukosefu wa umeme katika maeneo kadhaa ya Wilaya ya Tanga na kusababisha kero ya ukosefu wa huduma kwa wananchi,” alisema Makene.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Ofisa Usalama wa Tanesco mkoani Tanga, Emanuel Kimario alisema ameridhishwa na hukumu kwa kuwa vitendo hivyo vimesababishia hasara shirika ya zaidi ya Sh milioni 70.

“Shirika linalazimika kutumia fedha nyingi kurudisha huduma kwa wateja hali inayochangia kuzorotesha shughuli nyingine za kimaendeleo,” alisema Kimario.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live