Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana amuua baba yake na kutumia sehemu za mwili wake kutambika

PANGA Ed Kijana amuua baba yake na kutumia sehemu za mwili wake kutambika

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Usalama cha Jimbo la Ogun, nchini Nigeria kilichopewa jina la So-Safe Corps, kimemkamata kijana mwenye umri wa miaka 20 aliyetambulika kama Ridwan kwa madai ya kumuua baba yake kwa madhumuni ya ibada za kiasili (matambiko) huko Ogun.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwenye Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha usalama nchini humo, ilisema kuwa mnamo Agosti 31, maofisa wa Kikosi hicho waliokuwa katika doria ya kawaida na ndipo waliposikia kelele za ajabu kwenye jengo wakiwa katika Kijiji cha Oshoku kwenye Halmashauri ya Ijebu Kaskazini.

Maofisa hao waliingia ndani ya jengo hilo kuthibitisha kinachoendelea, lakini kwa mshangao, walikuta mwili wa mtu ukiwa umelazwa kwenye damu na mtu anayedaiwa kuwa ni muuaji alikimbia eneo la tukio.

Mshukiwa wa mauaji alinaswa alipokuwa amejificha kwenye kichaka; “Alikiri kumuua baba yake Ishau kwa kumfunga kamba shingoni na kisha kutumia kisu kutoa sehemu zinazohitajika za mwili wake kwa ajili ya ibada ya tambiko".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: