Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana akutwa amechinjwa porini

C6F8D6F6 5ED3 49E6 8B76 BEC11E207A30.jpeg Kijana akutwa amechinjwa porini

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja aitwae Richard Busagosya, umri wa Miaka 18 Mkazi wa kijiji cha Msasa Kata ya Msasa Tarafa ya Busanda wilayani Geita Mkoani Geita ambaye alikuwa akichunga Ng’ombe katika Pori la Samina amekutwa amekufa akiwa amechinjwa .

Inadaiwa chanzo cha kijana huyo kuchinjwa ni migogoro kati ya wafugaji na wakulima ambapo mgogoro huo umedumu kwa mda mrefu.

Kwa upande wake Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Msasa pamoja na Diwani wa kata ya Busanda, Seleman Gamala amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kufika katika eneo hilo huku akiwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani inahatarisha maisha ya wananchi wenzao.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live