Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana ahukumiwa viboko 6 kwa kumbata binti wa miaka 13

Cosmas Hango Kijana ahukumiwa viboko 6 kwa kumbata binti wa miaka 13

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro imemhukumu adhabu ya viboko sita Cosmas Hango (18) kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13 kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo imetolewa chini ya kifungu Namba 131 kifungu kidogo cha pili A cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya 2022.

Katika shauri hilo la Jinai Namba -99/2023, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 9, 2023 katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika mji mdogo wa Gairo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Gairo, Victor Kitauka amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kujiridhisha na ushahidi wa pande zote mbili.

Adhabu ya viboko sita imetolewa kutokana na mshtakiwa kuwa na umri wa miaka 18 na kwamba hana rekodi ya kutenda makosa mengine ya jinai.

Ilielezwa mahakamni hapo kuwa mshatikiwa alimshawishi binti huyo kufanya mapenzi ambapo binti alitoroka nyumbani kwao na kwenda na mshtakiwa katika nyumba ya kulala wageni, ambapo dada wa mhanga akiwa na askari polisi walipata taarifa kwa wasamaria wema na kumkamata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live