Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana adaiwa kumuua baba yake

Muuaji Md Adaiwa kumuua baba yake

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Nairobi imemzuilia kwa siku tano, mwanamume anayeshukiwa kumuua baba yake huko Kibera huku uchunguzi ukiendelea.

Joseph Atero Nanzai alizuiliwa na hakimu wa mahakama ya Kibera Jaqueline Ojwang baada ya koplo Peter Kariuki kuwasilisha hati ya kiapo mahakamani.

Mahakama ilisikia kuwa mshukiwa huyo kwa nyakati tofauti alitoa vitisho na na kuapa kumuua babake Amos Nanzai Okaalo kabla ya kifo chake cha ghafla.

"Marehemu ni babake mshtakiwa na walikuwa wakiishi pamoja katika nyumba yao katika kitongoji duni cha Kibera," afisa huyo aliambia mahakama.

"Kwa nyakati tofauti ametishia kumuua babake na chifu wa eneo hilo na wazee wa Nyumba Kumi walilazimika kuingilia kati."

Aliiambia mahakama kuwa taarifa ya kupotea kwa mtu huyo ilitolewa katika kituo cha polisi cha Langata chini ya OB Namba 22/02/02/2023, hata hivyo siku mbili baadaye ilitolewa namba nyingine ya OB namba 4/02/022023 ambayo ilionyesha kuwa mtu huyo amekamatwa kuuawa.

Mahakama ilisikia kwamba mwili wa mwanamume huyo uligunduliwa baada ya harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake.

"Kulikuwa na harufu mbaya kutoka kwa nyumba ya marehemu na alipofungua mlango alikutwa kitandani akiwa hana uhai na damu ikitoka mdomoni, marehemu hakuwa dhaifu wala mgonjwa kabla ya kifo chake,” Kariuki aliambia mahakama.

Afisa wa upelelezi aliitaka mahakama kumpa siku zaidi za kukamilisha upelelezi kwani washukiwa wengine muhimu bado hawajarekodi maelezo yao.

Pia aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alihitaji kufanyiwa uchunguzi wa kiakili ili kubaini iwapo ana uwezo wa kujibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live