Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana adaiwa kulawitiwa kisha kuawa Arusha

Kifo Kifo Mauiaji.png Kijana adaiwa kulawitiwa kisha kuawa Arusha

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la Henry Tumaini Lekule (34) amefariki dunia Mkoani Arusha kwa kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kichwani, Pamoja na kutobolewa macho huku pia ikielezwa alilawitiwa kabla ya kuuawa.

Kulingana na Familia ya Mzee Tumaini Lekule amesema tukio hilo limetokea usiku wa jumapili ya kuamkia jumatatu ya Februari 12, 2024, eneo la Block D, Njiro jijini Arusha.

Inaelewa na Familia kuwa mwili wa mpendwa wao waliukuta eneo la wazi lililopo karibu na nyumbani, ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali, na polisi waliuchukua kwaajili ya uchunguzi.

Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na Wivu wa kimapenzi, ikidaiwa Henri aliwahi kumfumania mkewe ambaye alimshawishi kuhama kwao na kuhamia ukweni, huku wakijaaliwa Watoto wawili kati ya watatu aliozaa mkewe.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live