Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo wizarani alimwa faini Sh2.9 milioni

Ceo D . Law Kigogo wizarani alimwa faini Sh2.9 milioni

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Easter Riwa amehukumiwa kulipa faini ya Sh2.9 milioni au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kufanya ubadhirifu wa fedha za wizara hiyo.

Pia mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa huyo kurudisha kiasi cha Sh 2.9 milion kwenye wizara hiyo zilizotakiwa kulipa posho za maofisa wa maendeleo ya vijana mkoani Ruvuma.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu Januari 30, 2023 na Hakimu Mkazi mkuu, Pamela Mazengo aliyesema mshtakiwa ametiwa hatiani kwa mashtaka 21 Kati ya hayo 19 ya kughushi, moja la ubadhirifu na moja la kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajili wake.

Mazengo amesema mashtaka 19 ya kughushi kila moja anatakiwa alipe faini ya Sh100,000 au kwenda jela mwaka mmoja, huku shitaka la ubadhirifu akitakiwa alipe faini ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja na shitaka la kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake mshtakiwa huyo anatakiwa kulipa fidia ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Amesema mshitakiwa huyo akimaliza kifungo chake anatakiwa ailipe Wizara hiyo Sh2.9 milioni fedha kwa ajili ya malipo ya posho za maofisa wa maendeleo ya vijana wa mkoani Ruvuma ambazo.

"Mshitakiwa anatakiwa kulipa fidia kwa kila kosa ambapo jumla yake ni Sh2.9 milioni na kila kosa anatakiwa afungwe mwaka mmoja lakini vyote vitakwenda kwa pamoja ambapo kifungo chake no mwaka mmoja," amesema Mazengo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live