Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo wizara ya fedha akutwa amekufa Mkuranga

68761 Pic+kigogo

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.

Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.

“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.

Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli. Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.

Chanzo: mwananchi.co.tz