Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo wa Acacia apandishwa kizimbani

23604 Accasiana+pic TanzaniaWeb

Wed, 24 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Acacia Tanzania, Asa Mwaipopo (55) amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka tisa yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Mwaipopo amepandishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka yanayomkabili leo Jumanne Oktoba 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi na Jacqline Nyantole, amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kwamba wanaomba kumuunganisha katika ya kesi uhujumu uchumi inayowakabili washtakiwa sita akiwemo aliyekuwa rais wa migodi hiyo, Deogratias Mwanyika (56).

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ambao walisomewa mashtaka 39, Oktoba 17, 2018 mahakamani hapo ni Meneja Mawasiliano wa Mgodi wa Bulyanhulu, Alex Lugendo (41) ambaye pia ni mkazi wa Dar es Salaam.

Washtakiwa wengine ni kampuni za migodi ya madini za Pangea Ltd,  North Mara, Exploration Du Nord LTEE na Bulyanhulu.

Nchimbi amedai Mwaipopo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Migodi ya Pangea Mineral Ltd,  Bulyanhulu na North Mara anakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha,  kughushi, kukwepa kodi na kuongeza uhalifu wa kupanga.

Anadaiwa katika shtaka la kwanza ambalo ni kula njama, linalowakabili Mwanyika na Lugendo na Mwaipopo, Wakili Nchimbi alidai katika tarehe tofauti kati ya April 11,  2008 na Juni 30, 2017 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam;  Kahama; Tarime na Biharamulo pamoja na maeneo mbalimbali ya mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini; Toronto nchini Canada; visima vya Barbados na nchini Uingereza walikula njama ya kutenda kosa la kughushi na kukwepa kodi.

Wakili Nchimbi amedai katika shtaka la pili Mwanyika, Lugendo na Mwaipopo wanadaiwa siku hiyo katika maeneo hayo waliongoza kusaidia kutenda uhalifu.

Pia  Mwanyika,  Lugendo na Mwaipopo wanadaiwa kati ya Aprili 11, 2008 na Mei 29, 2008 maeneo hayo, kwa nia ya kulaghai walighushi mkataba wa makubaliano ya  mkopo wakitaka kuonyesha kuwa Mgodi wa Madini wa Pangea ulikubali kukopa mkopo wenye riba wa Dola 90 milioni kutoka Barrick International Bank Corp,  wakati wakijua kuwa si kweli.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz