Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo tata mwanafunzi anayedaiwa kujinyonga kisa gari ya shule

Crime Scene 45.jpeg Kifo tata mwanafunzi anayedaiwa kujinyonga kisa gari ya shule

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alex Saleh Mgonja (11) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi ya Mother Kelvin Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro anadaiwa kufariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni katazo la kupanda gari la shule.

Mwanafunzi huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kitenge cha bibi yake huku kifo chake kikitajwa kuwa na utata kwa taarifa zinazodai kuwa huenda uamuzi huo umetokana na uwepo wa katazo la kutopanda gari la shule endapo hatalipa ada.

Hata hivyo, mwanafunzi huyo ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Majengo, Kata ya Stesheni hakwenda shuleni siku ya Julai 5 baada ya kuambiwa kuwa hataruhisiwa kupanda gari kutokana na hajalipa ada ya muhula wa pili wa masomo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amesema tukio hilo limewasikitisha huku akitaka wazazi kuwa karibu na watoto wao na sio kuwaachia ndugu wengine kuwalea.

"Ni kweli kuna mtoto wa darasa la tano alikuwa anadaiwa ada shuleni, kwa hiyo akawa amemwambia mzazi wake kwamba anaomba apewe ada ili apeleke shuleni lakini mama yake alimwambia asubiri baada ya muda flani atapata hizo fedha na atalipa ada,"

Amesema mtoto huyo alikuwa haishi na wazazi wake tangu utotoni na kwamba alikuwa akiishi na bibi yake mzaa baba siku zote.

"Sasa huyu mtoto huku Same anakaa na bibi yake na hizi fedha za ada inaonekana huyu mzazi wake yuko nje ya Same sasa sijajua kulitokea malumbano au ilikuwaje, lakini huyu mtoto alikuwa akimwambia dada yake wa kazi atajinyonga hivyo hiyo siku alipata sehemu ya kujinyongea akawa amejinyonga,"

"Ni tukio ambalo limetusikitisha sana, lakini niwaombe wazazi maana familia nyingi unakuta wazazi wako mbali na watoto na wanabaki na bibi zao na wakati mwingine wazazi wanawasahau hawa watoto na wanakaa kwenye mazingira magumu, unakuta hata kama mtoto ana ule moyo wa kusoma unaisha,"

"Nitoe wito kwa wazazi kama tulivyokuwa katika mazingira mazuri ya kupata hawa watoto basi tuhakikishe tunawapa haki zao za msingi za elimu na kuwalinda watoto dhidi ya mazingira yoyote ambayo yatamfanya mtoto ashindwe kupata elimu, naomba wazazi tuwe karibu na watoto wetu na familia zetu," amesema.

Naye, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo, Joyce Mndeme amesema kwa taarifa za dada wa kazi wa nyumbani alikokuwa akiishi mwanafunzi huyo alidai kuwa mwanafunzi huyo amekuwa akitamka mara kadhaa kujua bila kueleza sababu za kutaka kufanya hivyo ni nini.

Hata hivyo Mndeme amesema baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo kutengana mwanafunzi huyo tangu akiwa mdogo alikuwa akiishi na bibi mzaa baba kwa miaka yote mpaka hapo alipojiua.

"Huyu mwanafunzi muhula huu alikuwa hajalipiwa ada, sasa ile siku ya Jumanne alimwambia bibi yake kuwa, kwenye gari ameambiwa hatapanda gari la shule siku hiyo ya Jumatano maana hajalipiwa ada na bibi yake akamwambia sawa hakuna shida wewe tulia kwasababu Ijumaa ni sikukuu baba amesema atakulipia, hivyo kabla hajalipiwa ada alifanya maamuzi ya kujinyonga,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live