Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiapo chaibua utata kortini

Hukumu Pc Data Kiapo chaibua utata kortini

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiapo kinzani cha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na wenzake katika shauri la maombi ya uchunguzi wa kifo cha mwanamke aliyedaiwa kujinyonga katika mahabusu ya kituo cha Polisi Mburahati kimeibua utata mahakamani, baada ya wakili wa familia ya marehemu kukistukia.

Mwanamke huyo, Stella Moses alifariki dunia Desemba 20, 2020, akiwa mahabusu kituoni hapo alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika.

Mwishoni mwa wiki Wakili Peter Madeleka aliieleza Mahakama kuwa nakala ya kiapo kinzani walichopewa hakionyeshi kama kimewasilishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Matumizi ya Sheria Mbalimbali.

Alidai kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, kiapo cha pamoja cha wajibu maombi hao kimewasilishwa mahakamani hapo isivyo sahihi, hivyo wajibu maombi hayo hawakutekeleza amri ya Mahakama ya Juni 28, mwaka huu.

Aliiomba Mahakama hiyo ione hakuna kiapo kinzani cha wajibu maombi hao na kisha ipange tarehe ya usikilizwaji wa maombi hayo.

Kwa mujibu wa polisi, mwanamke huyo alijinyonga lakini ndugu wa marehemu walipinga taarifa hiyo wakidai kuna utata wa kifo hicho.

Advertisement Machi mwaka huu, familia kupitia shemeji wa marehemu, Emmanuel Kagongo ilifungua shauri la maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam Kivukoni (Kinondoni), akiiomba iamuru ufanyike uchunguzi huru kujua ukweli wa mazingira ya kifo hicho.

Mbali na IGP, wajibu maombi wengine katika shauri hilo namba 3 la mwaka 2022 ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC) na Kamanda wa Polis Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RPC).

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mburahati (OCD), Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Juni 28 mahakama hiyo iliwaamuru wajibu maombi wa kwanza mpaka wa nne kuwasilisha mahakamani viapo kinzani vyao baada ya kuwaongezea muda kutokana na kushindwa kuwasilisha viapo hivyo awali kwa muda uliotakiwa.

Akijibu hoja za Wakili wa Serikali, Daisy Makakala alisema kuwa nakala waliyoiwasilisha mahakamani imefuata utaratibu zote za kimahakama na kwa wakati.

Alidai baada ya kuwasilisha mahakamani nyaraka hiyo, walimtumia wakili Madeleka kwa baruapepe lakini ameomba moja ya nakala alizosailia nazo kwa madai kuwa yeye hakuwahi kuziprint.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live