Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi yashindwa kuendelea mshtakiwa kalazwa Muhimbili

Mon, 17 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Shirika la Reli (RAHCO) baada ya mshtakiwa wa pili mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).

Wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mshtakiwa wa pili anaumwa na amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

"Shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi tunaye hapa lakini mshtakiwabwa pili anaumwa hivyo naiomba mahakama hii ipangebtarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa," alidai Ndimbo

Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka siku ya shauri hilo linapokuja mahakamani hapo waje na shahidi mwingine ili aweze kutoa ushahidi pindi shahidi wa kwanza atakapomalizia kutoa ushahidi wake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24 na Juni 25,2019 itakapokuja kwa ajili ya ushahidi.

Mbali na Mwinyijuma washtakiwa wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito; Mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo na Mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe.

Pia Soma

Katika kesi hiyo tayari shahidi mmoja kwa upande wa mashtaka Regnald Malele ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC),ametoa ushahidi hata hivyo hajamaliza kutoa ushahidi wake.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane ikiwamo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kuisababishia Rahco hasara ya dola za Marekani 527,540,000.

Chanzo: mwananchi.co.tz