Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya wanaodaiwa kumbaka mtoto, kuiba kusikilizwa Agosti 29

71986 Ubakajipic

Mon, 19 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala Agosti 29, 2019 itaanza kuisikiliza kesi ya  kuvunja, kuiba na  kubakwa kwa mtoto wa miaka 15 inayowakabili  washtakiwa,  Omary Mussa (30) na Maulid Juma (20).

Wakili wa Serikali, Anna Chimpae mwishoni mwa wiki iliyopita amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Adolf Sachore kuwa katika usikilizwaji wa kesi hiyo upande wa mashtaka wanatarajia kuwaita mashahidi saba kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Hatua hiyo ilifikiwa mahakamani hapo baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo na washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Akiwasomea maelezo hayo, Chimpae amedai Juni 26, 2018  eneo la Pugu Kajiungeni washtakiwa walivunja nyumba ya Elizabeth Zacharia na kutenda kosa.

Chimpae amedai mbali na kuvunja nyumba hiyo, washtakiwa hao waliiba  simu mbili aina ya Tecno na zenye thamani ya Sh480,000  na fedha taslimu Sh20,000

 mali ya Elizabeth Zacharia.

Pia Soma

Mbali na mashtaka hayo, Chimpae amedai mahakamani hapo kuwa siku ya tukio washtakiwa walimbaka mtoto huyo.

Washtakiwa hao walikubali maelezo yao binafsi ikiwemo majina yao, shughuli zao na  wanapoishi na kuyakana mashtaka yanayowakabili.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz