Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya wanafunzi wa KIU kumdhihaki Rais Magufuli kuendelea Oktoba 8

74446 Kiu+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya Ilala Oktoba 8, mwaka huu, itaendelea kuisikiliza kesi inayowakabili mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala Tanzania.

Wanafunzi hao wanakabiliwa na shtaka la kusambaza picha kupitia mtandao wa WhatsApp ikimuonyesha Rais wa Magufuli akiwa amevaa hijabu.

Wakili wa Serikali, Grace Lwila leo Septemba 5, 2019 alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Fadhili Luvinga kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, lakini hawana shahidi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Luvinga aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 8, mwaka huu na mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo.

Wanafunzi wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Amenitha Konga (19), Mariam Twelve (20) na Agnes Gabriel (21) wote wanatetewa na wakili Alphonce Nachipyangu.

Katika kesi hiyo, washtakiwa na mshtakiwa mwingine, Anene Mwansasu (23) ambaye hana kazi, kwa pamoja wanadaiwa kuwa Juni 9, 2016 ndani ya jiji la Dar es Salaam walichapisha taarifa ya uongo kupitia mfumo wa kompyuta.

Pia Soma

Advertisement
Na walisambaza kwenye mtandao wa WhatsApp picha ikimuonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu vazi linalovaliwa na wanawake wa dini ya Kiislamu. Washtakiwa wote wako nje kwa dhamana.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz