Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya viongozi wa CCM yakwama, kuendelea Agosti 2019

67756 Pic+takukuru

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayowakabili viongozi watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala nchini Tanzania itaanza kusikilizwa Agosti 21, 2019 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh5 milioni na kupokea Sh3 milioni. 

Viongozi hao ni Jenifer  Mushi ambaye ni Katibu wa CCM Tawi la Amana(47), Devotha Batulake Katibu Kata CCM Ilala (43) na Frank Mang'ati ambaye ni Katibu Hamasa CCM Mkoa wa Dar es Salaam(38).

Kesi hiyo ilipaswa kuanza kusikilizwa leo Jumatatu Julai 22, 2019 kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka lakini imeshindikana baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Veronica Chimwanda kueleza mbele ya Hakimu Mfawidhi Martha Mpaze kuwa hawana shahidi.

Hivyo, Hakimu Mpaze ameiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 21 mwaka 2019 ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka wataanza kutoa ushahidi wao.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Takukuru kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo na washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).

Pia Soma

Katika kesi hiyo ya jinai namba 250 ya mwaka 2019 washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa Machi 21, 2019, Klabu ya Wazee Amana, Dar es Salaam  walishawishi Rushwa ya Sh5 milioni kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Daluni  East Africa Transport, Daud Kalaghe ili waweze kumpatia kiwanja namba 41 Y kinachomilikiwa na CCM kwa shughuli ya biashara.

Inaendelea kudaiwa kuwa Machi 22, 2019 katika eneo la Msimbazi Sekondari washtakiwa hao walijipatia rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Daluni  East Africa Transport, Daud Kalaghe ili waweze kumpatia kiwanja namba 41 Y kinachomilikiwa na CCM kwa shughuli ya biashara. Kitu ambacho kinahusiana na shughuli za mwajiri wao.

Washtakiwa  hao, wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha  masharti ya kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh5 milioni.

Washtakiwa hao walikamatwa Machi 21, 2019 baada ya kuwekewa mtego na Takukuru.

Chanzo: mwananchi.co.tz