Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya vigogo Chadema, Polisi aiambia korti walirusha risasi 90

57357 Pic+polisi

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shahidi wa Serikali katika kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wanane ameeleza kuwa polisi walifyatua risasi zaidi ya 90 kuzuia waandamanaji.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni katibu mkuu, Vincent Mashinji; naibu katibu mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu; naibu katibu mkuu bara, John Mnyika; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Tarime Mjini; Ester Matiko; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Tarime Vijijini; John Heche.

Shahidi huyo ambaye ni mkuu wa operesheni Mkoa wa Polisi Kinondoni, Gerald Ngichi ameeleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya wakili wa utetezi, John Malya kutaka kufahamu idadi ya risasi zilizofyatuliwa.

Ngichi alidai waandamanaji walikuwa zaidi ya 500 na waliokamatwa ni waandamanaji 43. Baadhi ya mahojiano baina ya wakili Malya na shahidi huyo yalikuwa hivi:

Wakili Malya: Unasema mliwakamata waandamaji 43 ni yupi alikutwa na risasi?

Shahidi: Hakuna

Pia Soma

Wakilli Malya: Askari wako uliwaamuru warushe risasi hewani walitumia silaha ya aina gani?

Shahidi: AK 47.

Wakili Malya. Ak47 risasi yake ikipigwa inaenda wapi?

Shahidi: Inaenda hewani.

Wakili Malya: Ulikuwa unasimamia operesheni ulikuwa unajua hizi risasi zinarejea kwenda chini zilikuwa zikienda upande gani.

Shahidi: Ardhini

Hakimu Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hadi leo.

Chanzo: mwananchi.co.tz