Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya usafirishaji haramu watu 95 yaendelea kuunguruma Kisutu

Aabf1955e584b9b7e321f88949a9797d.jpeg Kesi ya usafirishaji haramu watu 95 yaendelea kuunguruma Kisutu

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa utetezi katika kesi inayomkabili raia wa Misri, Mohamed Shalaby anayekabiliwa na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watu 95 kukamilisha maombi waliyotoa kwa mahakama hiyo ili kesi hiyo iendelee kwa hatua nyingine.

Agizo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya anayesikiliza kesi hiyo wakati mshtakiwa huyo ilipopelekwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi kukamilika.

Kabla ya uamuzi huo, mwendesha mashtaka kutoka Idara ya Uhamiaji, Godfrey Mbwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa, kesi hiyo ilipelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali, lakini siku moja kabla upande wa utetezi ulipeleka maombi ya mshtakiwa kubadili msimamo wa kukana mashitaka yake.

"Shauri hili limekuja kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali, lakini jana (juzi) upande wa utetezi ulileta maombi ya mshtakiwa kubadili nia ya kukana mashtaka na waliomba muda waweze kujadiliana, hivyo tungependa kujua wamefikia wapi," alisema Mbwijo.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Utetezi, Magusu Mugoka alisema bado wapo katika majadiliano na ndugu wa mshtakiwa na bado hawajafikia mwafaka hivyo wanaomba kupewa tarehe nyingine.

Upande wa mashtaka ulikubaliana na ombi hilo, lakini uliiomba mahakama kuwa, kesi hiyo itakaporejea wawe wameshakubaliana na kutekeleza ombi lao, kinyume cha hapo watasoma maelezo ya awali kwa mshtakiwa na kuanza kusikiliza shahidi wa kwanza siku hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Shalaby anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji haramu wa binadamu kosa analodaiwa kulitenda Agosti 4, mwaka huu katika eneo la makazi la Avone, Ilala, Dar es Salaam akiwa ni raia wa Misri na Mauritania alikutwa akisafirisha watu 95 kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa, kati ya watu hao, 90 ni raia wa Tanzania na watano ni raia wa Burundi.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba Mosi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz