Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya upatu, kutakatisha fedha yapigwa kalenda

34242 Pic+kesi Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Upelelezi wa kesi ya kufanya biashara ya upatu na kutakatisha fedha inayowakabili wakurugenzi wa kampuni ya Rifaro Africa Limited, Jones Moshi(42) na James Gathonjia(35) bado haujakamilika.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh1.022bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Desemba 31, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wakili wa Serikali,  Neema Mbwana mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mbwana imedai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado unaendelea hivyo ameiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi  Januari 10, 2019.

Katika shtaka la kwanza kati ya Julai 14, 2014 na Julai 31, 2016 jijini Dar es Salaam na maeneo mbalimbali nchini Tanzania, washtakiwa hao walipanga njama ya kuendesha biashara ya upatu.

Katika shtaka la pili, wanadaiwa katika kipindi hicho na maeneo hayo washtakiwa hao wanadaiwa kuwa waliendesha biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi kuwa fedha hizo zitazaa.

Shtaka la tatu la utakatishaji wa fedha, inadaiwa  kuwa katika kipindi hicho washtakiwa hao walijihusisha na miamala ya fedha moja kwa moja ya Sh1,022, 560, 854 kupitia akaunti namba 3301106013 iliyopo katika benki ya KCB yenye jina la Rifaro Africa Limited wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuendesha biashara ya upatu.



Chanzo: mwananchi.co.tz