Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya uhujumu uchumi yaahirishwa washtakiwa wakirudi rumande

Uhujum Uchumi Pic Kesi ya uhujumu uchumi yaahirishwa washtakiwa wakirudi rumande

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imehairisha kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayowakabili wafanyabiashara 10 wa madini ya dhahabu hadi Julai 31, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo namba 4/2023 iliyopangwa leo Jumatatu Julai 17, 2023 kwaajili ya kutajwa, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Washtakiwa hao ni Makaranga Bukene, Sindano Robert, Bahame Kisinza, Hassan Juma, Sungwa Mbusi, Sondi Misuzi, Yusufu Mamboleo, Ramla Ahmed, Mageme Ntobi na Geodfrey Joseph.

Akiomba tarehe ya ahirisho hilo kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Scollastica Teffe ameielezea kuwa uchunguzi haujakamilika na kuiomba kutoa tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Wafanyabiashara hao wanadaiwa kutenda makosa hayo maeneo tofauti ya mikoa ya Shinyanga, Geita, Mwanza na Dar es Salaam katika siku tofauti kati ya Februari Mosi, 2018 na Juni Mosi 2023.

Miongoni mwa makosa yanayowakabili ni pamoja na kuunda genge la uhalifu na kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo biashara haramu ya madini kinyume na kifungu cha 18 (1)(4a) ya sheria ya madini na aya ya 27 jedwali la kwanza kifungu cha 57(1)(2) cha sheria ya Uhujumu Uchumi.

Wanadaiwa kuhujumu uchumi kwa kufanya biashara ya kuuza dhahabu kilo 2,348 zenye thamani ya Sh345.9 bilioni bila kuwa na leseni pamoja na kuisababishia tume ya madini hasara ya Sh24.2 bilioni ambazo ni mapato kupitia mrabaha na tozo ya ukaguzi wa madini.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shauri hilo kutokuwa na dhamana na itakuja tena mahakamani Julai 31, 2023 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live