Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya tajiri Zakaria kizungumkuti

10640 Kesi+pic TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma.  Mpaka sasa mfanyabiashara maarufu mkoani Mara, Peter Zakaria, bado hajafikishwa mahakamani.

Waandishi wa Mwananchi waliopiga kambi leo Julai 3 katika Mahakama ya Hakimu mkazi mjini Musoma wameshuhudia washtakiwa wengine wakifikishwa mahakamani hapo bila Zakaria kuwemo miongoni mwao.

Tofauti na jana ambapo ndugu, jamaa na marafiki wa Zakaria walionekana kuzunguka kwenye viunga na vyumba vya mahakama wakizungumza na makarani na watumishi wengine wa mhimili huo wa dola, leo pilika hizo hazipo si tu mahakamani, bali hata katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma anakoshikiliwa mfanyabiashara huyo.

Akizungumza na Mwananchi, Hakimu Mkazi, Rahimu Mushi amesema hadi saa 3:30 asubuhi, faili la shauri la Zakaria halikuwa limepokelewa mahakamani hapo.

"Kwa kawaida mafaili ya mashauri yote mapya yanapaswa kufika mahakamani kabla ya saa 3 asubuhi kwa ajili ya taratibu za kiutawala ikiwemo kupangiwa hakimu; hadi sasa sijalipokea faili lenye shtaka unaloliulizia," amesema Hakimu Mushi na kuongeza:

"Labda shauri hilo litakuja kesho maana muda wa kupokea na kupitia mafaili tayari umekwisha,"amesema.

Soma Zaidi:

Tajiri wa mabasi ya Zakaria ahojiwa kwa tuhuma za kuwapiga risasi maofisa usalama

 

Chanzo: mwananchi.co.tz