Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya picha za utupu, Mwijaku aachiwa huru

Mwijaku Conn Mwemba Burton maarufu kama Mwijaku

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii wa maigizo, Mwemba Burton maarufu Mwijaku, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake katika kesi ya kusambaza picha za utupu iliyokuwa inamkabili msanii huyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Mei 31, 2022 na Hakimu Mkazi, Rhoda Ngimilanga wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya hukumu.

Mwijaku alikuwa anakabiliwa na shtaka moja la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria, tukio analodaiwa kulitenda Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019, Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live