Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya ofisa wa Shirika la Posta yapigwa kalenda

Hukumu Pc Data Kesi ya ofisa wa Shirika la Posta yapigwa kalenda

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kesi inayomkabili aliyekuwa ofisa usalama wa Shirika la Posta Tanzania, Geogre Mwamgabe na wenzake wawili imeshindwa kuendelea na usikilizwaji kutokana na wakili wa upande wa utetezi kutokuwepo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 1.55 na bangi gramu 124.55.

Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa ushahidi na shahidi wanaye, wapo tayari kuendelea .

"Mheshimiwa tunaomba tuendelee kusikiliza ushahidi bila wakili kuwepo, kwa kuwa shahidi tuliyenaye ratiba yake imebana na tumefanya kazi kubwa sana kumpata leo, tumeonyeshwa hata ratiba ya vikao vinavyomkabili, hivyo tunaomba tusikilize hasa ukizingatia kuwa ushahidi wake ni mfupi sana," alidai Wakili Mnzava.

Hata hivyo, baada ya kufanyika mawasiliano na wakili wa washtakiwa hao, aliomba ushahidi usiendelee mpaka atakapokuwepo mahakamani na akaomba ahirisho ili kesi hiyo isikikizwe leo.

Hakimu Kabate baada ya maelezo hayo, alisema mahakama haiwezi kulazimisha upande wowote kufuata upande mwingine hivyo aliwataka wajadiline na wakubaliane tarehe ambayo ni rafiki kwa wote, mawakili pamoja na shahidi wapatikane.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 2, 2023 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Mbali na Mwamgabe wengine ni dereva wa shirika hilo, Abrahamani Msimu na Sima Ngaiza.

Chanzo: mwanachidigital