Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya mwanafunzi anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi yaahirishwa

Wed, 24 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya ubakaji inayomkabili mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Mbezi, Juma Idd imeahirishwa hadi Novemba 8, 2018 itakapotajwa tena.

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Septemba 26,2018 kwa kosa la kumwingilia kimwili mwanafunzi wa kike wa darasa la tano (14) anayesoma katika Shule ya Msingi Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi huyo kwa sasa ana mimba ya miezi mitano na ameshaanza kliniki katika Zahanati ya Tegeta jijini humo.

Akisoma shtaka hilo leo Jumanne Oktoba 23,2018 mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai upelelezi haujakamilika hivyo alimuomba hakimu apange tarehe nyingine.

Hivyo Hakimu Mushi amesema upelelezi haujakamilika hivyo kesi hiyo litatajwa tena Novemba 8,2018.

Wakili wa Serikali Makakala alidai katika tarehe  tofauti kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka huu mshtakiwa alimwingilia  kimwili mwanafunzi huyo huku ukijua ni kosa la kisheria .

Mshtakiwa alikana kosa hilo hivyo yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na kila mmoja alisaini bondi ya Sh1 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz