Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya mke wa bilionea Msuya yakwama tena

Mke Wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita Kesi ya mke wa bilionea Msuya yakwama tena

Fri, 25 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mke wa aliyekuwa bilionea wa madini, marehemu Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake kwa kuwa mmoja wa wazee wa baraza ameshindwa kufika mahakamani kutokana na sababu za kiafya.

Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Revocatus Muyella.

Katika kesi hiyo iliyokuwa iendelee kusikilizwa ushahidi juzi mbele ya Jaji Edwin Kakolaki, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Genes Tesha na upande wa utetezi uliwakilishwa na Peter Kibatala na Nehemia Mkoko.

Katika kesi hiyo washitakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa kukusudia dada wa marehemu Msuya, Aneth Msuya Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam

Chanzo: www.tanzaniaweb.live