Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya meneja wa PSSSF, wenzake yapigwa kalenda

RUNGU Kesi hiyo itatajwa Aprili 5

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imeahirisha kesi inayomkabili Meneja wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wa mkoa wa Temeke, Rajabu Kinande na wenzake watano baada ya mshtakiwa mmoja pamoja na wakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mshtaka matano likiwamo la wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh60.8 milioni.

Wakili wa Serikali, Michael Ng'hoboko alieleza mahakama hiyo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi hata hivyo wamepewa taarifa mshtakiwa Rose Mabaka amefariki dunia.

"Leo hii tulipanga tuwasomee upya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hawa baada ya kupewa taarifa kuwa Mabaka amefariki dunia na pia mshtakiwa Mbonaheri na wakili wa upande wa utetezi hawajafika mahakamani hivyo naiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine,"alidai Ng'hoboko.

Awali mshtakiwa Kinande alidai kuwa wakili wao wa utetezi waliokuwa wakimtegemea kufika mahakamani hapo anaumwa hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi, Fadhil Luvinga aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 5, 2022 kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa upya mashtaka yanayowakabili.

Mbali na Kinande washtakiwa wengine ni Dk Ashura Kapera (36), Farida Mbonaheri (33), Mohamed Miraji (47) na Msafiri Raha

Katika kesi ya msingi inadaiwa kati ya Juni 16,2020 mtaa wa Gerezani wilaya ya Ilala washtakiwa hao kwa pamoja walivunja na kuingia kwenye duka na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 60,8 milioni mali ya Mohamed Soli,Anwar Hemed,Rashidi Hassan na Salehe Seleman.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live