Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya maofisa polisi wanaodaiwa kuua yaahirishwa

Watuhumiwa Mtwara (600 X 590) Kesi ya maofisa polisi wanaodaiwa kuua yaahirishwa

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis (25) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kesi yao kutajwa.

Washtakiwa hao wamefikishwa leo Jumanne Februari 8, 2022 wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Kesi hiyo imetajwa leo na kuahirishwa hadi Februari 22, 2022 itakaposikilizwa tena.

Washtakiwa wanaohusishwa na mauaji hayo ni ofisa Upelelezi (OC CID) Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS), Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza na Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Polisi, Marco Mbuta. Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live