Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kukutwa na sehemu za siri, chuchu yakwama

Hukumu Pc Data Kesi ya kukutwa na sehemu za siri, chuchu yakwama

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu imeshindwa kuanza usikilizwaji wa kesi ya kukutwa na viungo vya binadamu hususan sehemu za siri za kike baada ya shahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo inayomkabili mkazi wa Maswa mkoani Shinyanga, Salum Nkonja (23) ilipangwa kuanza kusikilizwa ushahidi leo Jumanne Julai 19, 2022.

Hata hivyo mahakama hiyo imeshindwa kuanza usikilizwaji baada ya shahidi aliyekuwa anatarajiwa kutokutokea mahakamani.

Mwendesha mashtaka, wakili wa Serikali, Mosie Kaima, ameileza mahakama hiyo kuwa shahidi huyo waliyekuwa wanamtegemea kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, hakuweza kufika kwa kuwa yuko Dodoma.

Hivyo wakili Kaima aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza usikilizwaji, ombi ambalo halikupingwa na upande wa utetezi.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Ramadhani Rugemalira anayesikiliza kesi hiyo amekubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka na ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 2, mwaka huu.

Advertisement Nkonja ambaye pia anafahamika kama Emmanuel Nkonja anakabili wa mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na viungo vya binadamu, zikiwemo sehemu za siri tano za kike na matiti, mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu na nyara za Serikali.

Kwa mujibu wa maelezo ya upande wa mashtama, mshtakiwa wakati akihojiwa na Askari Polisi baada ya kukamatwa alidai kuwa viungo hivyo alitumwa kuvipeleka Rufiji mkoani Pwani.

Hayo yalibainishwa na mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali, Adolf Verandumi, siku ya usikilizwaji wa awali ambapo mshtakiwa alisomewa muhtasari wa mashtaka yanayomkabili.

Nkonja alinaswa na viungo hivyo vya binadamu pamoja na shehena ya nyara za Serikali, Oktoba 30, 2017, katika stendi Kuu ya zamani ya Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani (Ubungo).

Nyara hizo za Serikali ni pamoja na sikio na pembe ya nyati; mikia mitano ya Nguruwe; uume tatu za fisi; yai moja la mbuni; ndege mmoja mkavu na kichwa kimoja cha Combra" alidai Verandumi na kuongeza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live