Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kubaka watoto watatu kusikilizwa Mei 27

57183 Pic+ubakaji

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Machi 27, mwaka huu itaisikiliza kesi ya kubaka watoto watatu wa kike wenye umri wa miaka 13 na 14 inayomkabili Ustadhi Salumu Kingo (66).

Wakili wa Serikali, Anna Chimpae alieleza mbele ya Hakimu Mkazi, Samweli Obasi kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini kwa bahati mbaya mashahidi hawakufika.

Kutokana na hali hiyo, wakili huyo aliiomba Mahakama kuipangia tarehe nyingine kesi hiyo ili iendelee kusikilizwa.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, Hakimu Obasi aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 27, mwaka huu ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka wanaendelea kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo.

Katika kesi hiyo ya jinai, Ustadhi Salumu ambaye ni mkazi wa Vingunguti Koloni, Novemba 2, 2018 huko Buguruni Ghana katika wilaya ya Ilala alidaiwa kuwabaka watoto wa tatu wa kike wa umri wa miaka 13 na 14.

Chanzo: mwananchi.co.tz