Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kina Zumaridi yakwama tena

Zumaridiipic Data Kesi ya kina Zumaridi yakwama tena

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya jinai namba 10/2022 inayomkabili Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi na wenzake nane iliyotarajiwa kutolewa ushahidi wake wa upande wa utetezi jana imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa namba moja kudai kuwa ana maumivu ya mguu.

Mshtakiwa huyo ambaye ni Mfalme Zumaridi na wenzake nane wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya askari wa polisi na kuzuia maofisa wa serikali kutekeleza majukumu yao.

Akitoa maelezo ya kesi hiyo, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Martha Mwademi ameieleza mahakama kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa mashahidi wa utetezi baada ya Jamhuri kufunga ushahidi wake.

Hata hivyo, lengo hilo halikufikiwa baada ya wakili wa utetezi, Erick Mutta kusimama na kuieleza mahakama kuwa hawawezi kuendelea na ushahidi kwa sababu mteja wao hajisikii vizuri kutokana na majeraha aliyoyapata mguuni wakati analetwa mahakamani hapo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Hakimu Mkazi anayesikiliza shauri hilo, Monica Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19 mwaka huu itakapoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live