Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kina Sabaya yakwama tena

Video Sabaya Pic Data Kesi ya kina Sabaya yakwama

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imekwama kuendelea kusikilizwa kutokana na Hakimu anayeisikiliza kuwa na majukumu mengine ya kiofisi.

Leo Alhamisi Machi 10, 2022, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilipanga kuendelea kusikiliza shauri hilo namba 27/2021 kwa shahidi wa tano wa utetezi ambaye pia ni mshitakiwa wa sita, Jackson Macha (30) kuendelea kujitetea.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Pamela Meena alieleza kuwa Hakimu Mkazi Mwandamizi Patricia Kisinda, anayesikiliza shauri hilo bado anaendelea na majukumu ya kiofisi hataweza kuendelea kulisikiliza hadi Jumatatu Machi 14, 2022.

"Hakimu bado anaendelea na majukumu ya kiofisi hataweza kuendelea kusikiliza shauri hili kwa hiyo kesi itaendelea kusikilizwa Jumatatu,"amesema

Mahakama hiyo leo ilipanga kutoa uamuzi mdogo kufuatia maombi ya mshitakiwa wa tatu Watson Mwahomange, ambaye alishindwa kujitetea jana baada ya mawakili wanaowatetea washitakiwa wengine kuweka pingamizi kuzuia mahakama kutoa amri kwa Takukuru kumpatia simu yake aitumie kujitetea.

Jana Mwahomange aliomba mahakama iamuru Takukuru walete simu yake mahakamani hapo ili atumie kama kielelezo. Bonyeza hapa kusoma kilichojiri mahakamani jana

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live