Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kina Mbowe yakwama kuendelea

80194 Mbowepic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamepinga utaratibu wa mashahidi wa upande wa utetezi kuanza kutoa ushahidi kabla ya washtakiwa.

Pingamizi hilo limetolewa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Ni baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kesi ilipangwa ili kuona ni namna gani washtakiwa watatoa ushahidi wao.

Kibatala ameieleza mahakama washtakiwa watatoa ushahidi wao chini ya kiapo kwa kadri dini zao zinavyoruhusu.

Amesema katika kesi yao hiyo wataita mashahidi wengi na kwamba wanaye shahidi mmoja ambaye ataanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo.

Baada ya Kibatala kueleza  hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza hawana pingamizi na maelezo yaliyotolewa na wakili huyo ila changamoto ni shahidi kuanza kutoa ushahidi kabla ya washtakiwa.

Pia Soma

Advertisement
Nchimbi amedai utaratibu wa mashahidi kuanza kutoa ushahidi washtakiwa watoe baadaye unakinzana na miongozo ya kisheria na kwamba wanaupinga utaratibu huo.

Hata hivyo, Nchimbi ameongeza utaratibu huo hauna misingi ya kisheria unayoiunga mkono.

 

 

 

Baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili, Hakimu Simba ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 17, 2019 na akautaka upande wa mashtaka na utetezi wakasome sheria vya kutosha, wajadiliane na siku hiyo watoe hoja zao kuhusu utaratibu wa mashahidi kuanza kutoa ushahidi kabla ya washtakiwa.

Hakimu Simba amesema siku hiyo licha ya kuwasilishwa kwa hoja za pande hizo mbili pia upande wa utetezi utaanza kutoa ushahidi wao.

Washtakiwa hao wanaanza kutoa utetezi wao baada ya mashahidi  nane wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na Mahakama kuwaona washtakiwa hayo wana Kesi ya mujibu wajitetee.

Wanaokabiliwa katika kesi hiyo,  mbali na Mbowe  ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar- Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu katibu Mkuu Bara, John Mnyika.

Wengine ni wabunge; Halima Mdema (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Esther Matiko (Tarime Mjini) na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Shahidi kesi ya kina Mbowe ashindwa kumtambua mshtakiwa

Chanzo: mwananchi.co.tz