Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kina Mattaka kusikilizwa mfululizo

37740 Pic+mtaka Kesi ya kina Mattaka kusikilizwa mfululizo

Tue, 22 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga siku mbili mfululizo kuanzia Februari 27 hadi 28 kusikiliza ushahidi wa kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh71 bilioni, inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa ATCL, David Mattaka na wenzake wawili.

Uamuzi huo, ulitolewa jana na hakimu Augustino Rwezile wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi.

Hata hivyo, kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na shahidi ambaye alitakiwa kutoa ushahidi upande wa mashtaka kupata udhuru.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Vitalis Peter alidai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini shahidi ambaye walimpanga alipata udhuru, hivyo wanaomba terehe nyingine.

Peter baada ya kueleza hayo, wakili wa utetezi Omary Msemo aliomba upande wa mashtaka kuhakikisha wanapeleka mashahidi wengi ili mmoja asipofika, mwingine aendelee badala ya kuahirisha kesi.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hakimu Rwezile aliutaka upande wa mashtaka tarehe ijayo kupeleka mashahidi wa kutosha.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 27 itakapoendelea na ushahidi.

Tayari mashahidi 16 upande wa mashtaka wametoa ushahidi wao.

Inadaiwa Oktoba 9, 2007 Mattaka alisaini mkataba kukodisha ndege kwa ajili ya ATCL na Andrew Wettern kwa niaba ya kampuni ya Wallis Trading Inc na kwamba mkataba huo uliisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh71 bilioni.



Chanzo: mwananchi.co.tz