Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kigogo wa Chadema yaahirishwa

Kesi Kigogo Pic Data Kesi ya kigogo wa Chadema yaahirishwa

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi inayomkabili mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashimu Juma Issa (63) imeahirishwa baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuhamishwa katika mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Juma anakabiliwa mashtaka mawili la kuchapisha taarifa za uongo na uchochezi

Wakili wa Serikali,Adolf Lema alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Evodia Kyaruzi kuwa shauri hilo lilikuja kwaajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

"Shauri hili bado upelelezi bado haujakamilika na hakimu anayeendesha shauri hili amehamishwa hivyo naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Kyaruzi alisema hakimu anayeendesha shauri hilo hayupo hivyo anaahirisha hadi Novemba 19,2022 itakapokuja kwa ajili ya kutaja

Katika kesi hiyo ya jinai namba 179/2021 inadaiwa kuwa Oktoba Mosi mwaka huu, eneo la Kinondoni B mtaa wa Ufipa kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, mshtakiwa huyo alichapisha kwenye kompyuta na kusambaza ujumbe kwenye mtandao wa YouTube kuwa "Sirro ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi"

Katika shitaka la pili tarehe hiyohiyo, eneo la Kinondoni B mtaa wa Ufipa kwa lengo la kutengeneza chuki kwa wananchi wa Tanzania akitoa maneno ya uchochezi kuwa "Sirro ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live