Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya dhahabu: Washatakiwa wahukumiwa kulipa faini Sh230 milioni au kwenda jela miaka 15

74449 Dhahabu+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania imewahukumu kulipa faini ya Sh230 milioni au kufungwa miaka 15 jela washtakiwa wawili wa kesi ya uhujumu uchumi namba 8/2018 ya utoroshaji wa dhahabu nje ya nchi iliyokuwa inawakabili.

Pia, Mahakama imeamuru kutaifishwa kiasi hicho cha dhahabu kilo 35.34. waliohukumiwa adhabu hiyo ni Charles Warioba na Warioba Marwa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 5, 2019 na Hakimu Mkazi wa Mfawidhi wa Mkao wa Mwanza, Rhoda Ngimilanga baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka na kukiri kutenda makosa hayo.

Kabla ya Hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Shedrack Kimaro ameileza mahakama kuwa kutokana na mamlaka aliyonayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) ameipa kibali mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo baada ya upelelezi kukamilika.

Baada ya kusema hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Castus Ndamugoba aliwasomewa washtakiwa hao mashtaka matatu yanayowakabili ikiwa ni pamoja na kuongoza genge la uhalifu, kusafirisha madini kinyume na sheria na kosa la tatu ni kutakatisha fedha.

Baada ya kuwasomea mashtaka hayo, washtakiwa wote wawili kwa nyakati tofauti wamekiri kutenda makosa hayo.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Ndamugoba amedai washatakiwa walitenda makosa hayo kati ya Januari na Februari, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza na Nairobi nchini Kenya ambapo walikamatwa wakiwa na madini hao katika uwanja ndege wa Jomo Kenyatta Kenya.

Alidai walisafirisha madini hayo kinyemela kupitia uwanja wa ndege wa jijini Mwanza ambapo walikuwa na nia ya kuyasafirisha kwenda Dubai kuyauza.

Kabla ya Kutoa hukumu hiyo, Wakili wa serikali, Kimaro aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washatakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye kutenda makosa kama hayo na kwamba washatakiwa hao walitenda kukwepa kodi na kukosesha serikali mapato.

Nao mawakili wa utetezi, Makaki Masatu na Wilbeld Kilenzi walioomba mahakama kutoa adhabu kidogo wakidai washatakiwa hawajaisumbua mahakama.

Pia, Kilenzi amedai washatakiwa hao afya zao sio nzuri na kwamba wamekaa rumande zaidi ya mwaka mzima.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Ngimilanga amesema amezingatia maelezo ya pande zote mbili na kwamba kosa la kwanza kila mshatakiwa anatakiwa kulipa Sh5 milioni au kufungwa miaka mitano jela, kosa la pili kila mmoja alipe Sh10 milioni au kufungwa miaka 10 jela na kosa la tatu kulipa faini ya Sh100 milioni au kufungwa miaka 15 jela.

Makosa yote yanaenda kwa pamoja hivyo wakishindwa kulipa faini watatumikia kifungo miaka 15 jela kila mmoja. Washatakiwa hao wamepelekwa gerezani mpaka taratibu za kulipa zitakapokamilika.

Chanzo: mwananchi.co.tz