Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya anayedaiwa kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais Magufuli yapigwa kalenda

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais John Magufuli na kuzisambaza katika mtandao wa kijamii wa Facebook inayomkabili mfanyabiashara Henry Munisi imekwama kuendelea kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili wa Serikali, Sada Mohamed amedai leo Jumatano Februari 6, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaid kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

"Kesi hii imekuja kwaajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili haujakamilika tunaomba tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa,"amedai wakili Sada.

Hakimu Shahidi baada ya kusikiliza maelezo hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 6, 2019 itakapotajwa tena na mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.

Katika kesi ya msingi Munisi anadaiwa  Desemba 28, 2018 katika maeneo ya Veta jijini Mbeya alichapisha taarifa katika ukurasa wake wa Facebook kuwa 'Jinsi Magufuli alivyochota Sh1.5trilioni za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akitumia ujanja wa kuleta ndege ili atuibie', huku akijua taarifa hizo ni za uongo zenye nia ya kuupotosha umma.

Soma Zaidi: Kortini akidaiwa kumzushia Rais Magufuli uongo



Chanzo: mwananchi.co.tz