Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya aliyempa Waziri Lukuvi rushwa yagonga mwamba

11978 Pic+lukuvi TanzaniaWeb

Wed, 15 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara anayetuhumiwa kutaka kumpa rushwa ya Sh90 milioni Waziri William Lukuvi, bado haujakamilika.

Mfanyabiashara huyo, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Steal Group and Co. Ltd na Kiluwa Free Processing Zone anadaiwa kutaka kumpa rushwa hiyo Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hayo yameelezwa leo Agosti 15 na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huduma Shahidi wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili Ndimbo amedai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ili kuangalia kama ushahidi utakuwa umekamilika au la.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shahidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ambaye yupo nje kwa dhamana.

Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Julai 16, mwaka huu kati ya saa 6 na saa 8 mchana akiwa mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya Dola 40,000 za Marekani ( Sh90 milioni) kwa Waziri Lukuvi.

Chanzo: mwananchi.co.tz