Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya aliyekuwa mhasibu Takukuru kuendelea kesho

39963 Pic+gugai Kesi ya aliyekuwa mhasibu Takukuru kuendelea kesho

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesho Jumanne Februari 5, 2019 itaendelea kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato chake, inayomkabili aliyekuwa mhasibu mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai. Siku hiyo upande wa mashtaka unatarajiwa kuleta shahidi wa saba. Gugai na wenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo,  19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ya kumiliki mali zilizozidi kipato halali inayomkabili  Gugai. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera. Kwa mara ya kwanza Gugai na wenzake walifikishwa mahakamani Novemba 16, 2017 na walinyimwa dhamana kwa kuwa shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana. Tayari mashahidi sita wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi akiwemo mrajisi hati msaidizi wa wizara ya Ardhi, Joanitha Kazinja na msaidizi wa hati kanda ya Kaskazini kutoka wizara wa Ardhi, Emmanuel Bundala. Katika kesi ya msingi, Gugai na wenzake wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni ya kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai. Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo. Mbali na Gugai Mahakama hiyo pia itaendelea na ushahidi kwa upande wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya inayomkabili Linna. Lina anakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 43.95. Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 26, 2019 mwaka huu eneo la Tabata Bima kwenye nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii( NSSF).

Chanzo: mwananchi.co.tz