Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi Jiji la Arusha yavushwa tena

Pima Pic Data Kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi Jiji la Arusha yapigwa kalenda

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Mbali na Dk Pima watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022 ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya fedha katika halmashauri hiyo, Mariam Mshana na Mkuu wa Idara ya Mipango ya uchumi, Innocent Maduhu.

Leo Julai 5, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhil Mbelwa, kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa ambapo kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Juni 21, 2022 na kusomewa mashtaka sita katika kesi hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.

Baada ya maelezo hayo Wakili wa utetezi Valentine Nyalu, kutoka kampuni ya Maro Advocates ya jijini Arusha, aliyekuwa akiwatetea washtakiwa hao, aliieleza mahakama kuwa wamejiotoa katika uwakilishi wa watuhumiwa hao katika kesi hiyo.

Hii ni kesi ya tatu Wakili huyo kujitoa ambapo watuhumiwa hao wanaokabiliwa na kesi nyingine mbili za uhujumu uchumi, Julai Mosi mwaka huu, alijitoa kuwawakilisha watuhumiwa hao katika kesi zingine mbili zilizokiwa zinawakabili, bila kutaja sababu za kujitoa.

Baada ya kujitoa Wakili huyo, katika kesi hiyo watuhumiwa hao wanatetewa na Wakili Sabato Ngogo.

Katika kesi hiyo watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ikiwemo kosa la utakatishaji fedha Sh103 milioni, ambapo wanadaiwa kujipatia fedha hizo huku wakijua ni zao la uhalifu la kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Hakimu Mbelwa aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 14, 2022 itakapotajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live