Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida (45) na mkewe, Shamim Mwasha(41) umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania wanasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania.
Nsembo na Shamimu wakabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, kinyume cha sheria, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Wakili wa Serikali ya Tanzania, Wankyo Simon ameieleza Mahakama leo Jumatatu Juni 24, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Soma zaidi: Kilichojiri kesi ya Shamimu, mume wake hiki hapa
Simon ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina.
Pia Soma
- Mbunge Bwege adai wanyonge hawataichagua CCM 2020
- Bosi Udart, mkewe na wenzake kuendelea kusota rumande
- Profesa Kitila abainisha matatizo ya wahandisi kukwamisha maji vijijini
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 8, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.
Soma zaidi: Gramu 232 za heroine zawafikisha mahakamani Shamim Mwasha, mumewe
Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gram 232.70, wakati wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Mei mosi, 2019 katika eneo la Mbezi Beach, Jijini Dar Es Salaam.
Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa Kisutu, Mei 13, 2019.