Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Shamim, mmewe mambo ni yaleyale

69940 Pic+shamimu

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Upande wa mashtaka katika kesi  ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida (45) na mkewe, Shamim Mwasha (41) wamedai upelelezi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali ya Tanzania, Wankyo Simon amedai hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2019 mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Agosti 16, 2019 itakapotajwa tena.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam nchini Tanzania walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Mei 13, 2019.

Shamim na mumewe walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ambayo ni kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70

Pia Soma

Inadaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walisafirisha dawa hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz