Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sh1.6 bilioni za ABC kuanza kuunguruma

Hukumu Pc Data Kesi ya Sh1.6 bilioni za ABC kuanza kuunguruma

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajiwa kusikiliza mashahidi 11 pamoja na vielelezo 30 katika kesi ya wizi wa Sh1.6 bilioni mali ya benki ya ABC inayomkabili raia wa Ghana, Valentine Zacheus na Mtanzania, Fortunatus Bundala.

Akisoma maelezo ya awali Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilinyi alidai wawili hao wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama ya kutenda kosa la wizi.

Mbilinyi alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba Mosi, 2021 na Julai 31, 2022, washitakiwa hao walikuwa njama ya kutenda kosa la wizi.

Inadaiwa kuwa katika tarehe hizo washitakiwa hao walishirikiana na kufanikiwa kuingilia mfumo wa benki ya ABC na kuiba kiasi cha Sh1.6 bilioni

Anadai kwamba, uchunguzi ulifanyika washitakiwa hao walikamatwa na walipopekuliwa walikutwa na vitu mbalimbali ikiwemo simu na kompyuta ya mpakato.

Baada ya kusomwa maelezo hayo, washitakiwa hao walikana kutenda makosa hayo lakini majina yao na anwani za makazi yao pamoja na kupekuliwa walikubali.

Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi aliwataka upande wa mashtaka kuleta mashahidi ili shauri hilo liweze kwenda mbele.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 20, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live