Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Seth, Rugemalira upelelezi tatizo

46689 Seth+pic

Thu, 14 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayowakabili Habinder Seth na James Rugemalira imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upande wa Serikali wakamilishe upelelezi ili ushahidi uanze kusikilizwa.

Seth na Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi.

Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh309,461,300,158.27.

Hayo yamekuja baada ya Wakili wa Serikali, Iman Nitume kudai leo Alhamisi Machi 14, 2019 mbele ya mahakama hiyo kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Wakili wa Utetezi, Dora Malabu amedai shauri hilo lipo kwa muda mrefu hivyo aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi mapema ili ushahidi uanze kusikilizwa.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 28, 2019 na washtakiwa wamerudishwa rumande kwa kuwa shauri hilo halina dhamana.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo Juni 19, 2017, kujibu mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Rugemalira, ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Shtaka la pili la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam wakiwa si watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la tatu, Sethi anadaiwa kuwa Oktoba 10, 2011 katika mtaa wa Ohio, Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 ya usajili wa makampuni na kuonyesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau, Masaki wakati akijua ni uongo.

 Soma zaidi>>Kesi ya Rugemalira, Seth habari ni ile ile

    >> Upelelezi kesi ya Seth, Rugemalira haujakamilika

   >> Kesi ya Seth, Rugemalira yakwama tena



Chanzo: mwananchi.co.tz