Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sabaya yaendeshwa kwa njia ya mtandao

Sabaya Kesi Data Kesi ya Sabaya yaendeshwa kwa njia ya mtandao

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imeendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo Hakimu anayeisikiliza alikuwa Mahakama ya Wilaya ya Monduli huku washitakiwa na mawakili wa pande zote mbili wakiwa kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kilichopo kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 ilipangwa imeendelea kusikilizwa kwa Mawakili wa upande wa Jamhuri kuanza kumuuliza Sabaya maswali ya dodoso baada ya kumaliza kujitetea kwa kutoa ushahidi wake wa msingi Januari 21 mwaka huu.

Leo Februari 2, 2022 upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule na Wakili wa Serikali, Neema Mbwana huku utetezi ukiwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa na Fridolin Bwemelo.

Kesi hiyo imeendeshwa kwa njia ya mtandao ambapo kuliwekwa screen katikati ya chumba cha mahakama hiyo ambayo ilikuwa ikionyesha waliopo mahakamani hapo huku upande wa pili akionekana Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo.

Wakili Sekule ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho kwani kutokana na shughuli za kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, shauri hilo halikuweza kuendelea asubuhi.

"Shauri lilipangwa kwa ajili ya mshitakiwa wa kwanza ambaye pia ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi kuulizwa maswali ya dodoso ila kutokana na shughuli za law day, na muda sasa ni saa nane ikipendeza mahakama yako iahirishwe hadi kesho,"amesema

Hakimu Kisinda amekubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Februari 3, 2022 saa tatu na nusu asubuhi itakapoendelea.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo,Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Related Articles: