Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Sabaya ya Unyang'anyi Yafutwa, Mapya Yaibuka

Sabaya 1?fit=700%2C435&ssl=1 Kesi ya Sabaya

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kesi ya Sabaya ya Unyang’anyi Yafutwa, Mapya Yaibuka – Video July 16, 2021 by Global Publishers



KESI no 66/2021 ya Jamuhuri dhidi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Silivester Nyegu na Daniel Gabriel Mbula ya unyang’anyi wa kutumia silaha imefutwa katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Arusha baada ya wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka kuomba shuri hilo liondolewe katika mahakama hiyo leo Julai 16, 2021.

Wakili kweka ameomba shauri hilo kuhamishiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, ombi ambalo limekubaliwa na upande wa utetezi na Mahakama ambapo kesi hiyo imefutwa rasimi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi na kuhamishiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kupewa kesi no 105/2021 na imeanza kusikilizwa leo.

Sabaya na wenzake watano (katika mashtaka tofauti) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Arusha leo kwa mara ya nne wakikabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi, rushwa, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mbali na Ole Sabaya, washtakiwa wengine ni msaidizi wake wa karibu, Silvester Stanslaus, Enock Togolani, John Odemba, Daniel Gabriel Mbula, na Waston Mwakomange.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz